Huduma /

Ufungaji wa Pump na Solar Pump

Tunafunga submersible pump za umeme, solar pump na pampu za mkono, kulingana na wingi wa maji ya kisima chako.

Pampu sahihi inategemea kina cha kisima, wingi wa maji na kiasi unachohitaji kwa siku. Kwa kutumia matokeo ya pump test, tunachagua na kufunga pampu inayofaa: ya umeme (submersible), ya nishati ya jua (solar), au ya mkono kwa jamii.

Solar pump inakuondolea gharama ya umeme na inafanya kazi hata maeneo yasiyo na umeme wa gridi.

Hatua za kazi

  1. Kupima mahitaji ya maji kwa siku
  2. Kuchagua pampu na paneli za solar zinazofaa
  3. Kufunga pampu, mabomba na control box
  4. Kujaribu mfumo mzima
  5. Kukuelekeza jinsi ya kuutunza

Omba Huduma

Tuko tayari

Unahitaji kisima cha maji?

Tuambie ulipo na unachohitaji. Tutakupigia na kukupa makadirio ya gharama.