Kuhusu Milan Hydrotech

Wataalamu wa uchimbaji wa visima vya maji kwa mashine kubwa, utafiti wa maji ardhini, upimaji wa wingi wa maji (pump test), pampu na solar

Milan Hydrotech ni kampuni ya Kitanzania yenye makao makuu Mafinga, mkoani Iringa. Tunachimba visima vya maji kwa mashine kubwa za kisasa na kutoa huduma zote zinazohusiana na maji ya ardhini.

Kazi yetu huanza na utafiti wa maji ardhini unaofanywa na mtaalamu wetu wa jiolojia ya maji (hydrogeologist), ili kuchimba mahali penye maji ya kutosha. Baada ya uchimbaji, tunapima wingi na ubora wa maji, tunafunga pampu za umeme au za solar, tunajenga minara ya tenki, na tunakarabati visima vilivyoharibika.

Tunahudumia nyumba binafsi, mashamba, shule, taasisi, makanisa na misikiti, viwanda na jamii katika mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa, Dodoma na Singida.

  • Tangu: 2024
  • Mkurugenzi: Godfrey S. Mwambage
  • Ofisi kuu: Mafinga, Iringa, Tanzania
  • S.L.P: 655, Iringa
Milan Hydrotech

Timu Yetu

Watu wanaofanya kazi yako.

GS

Godfrey S. Mwambage

Mkurugenzi Mtendaji (CEO)

BG

Beatrice Godfrey

IM

Imani Mwamlenga

Mtaalamu wa Jiolojia ya Maji

AM

Abdalah Msimbe

Fundi (Technician)

DU

Denis Urasa

Fundi (Technician)

Mikoa Tunayohudumia

  • Iringa
  • Njombe
  • Mbeya
  • Dodoma
  • Singida

Uko nje ya mikoa hii? Tupigie, tutaangalia namna ya kukufikia.

Tuko tayari

Unahitaji kisima cha maji?

Tuambie ulipo na unachohitaji. Tutakupigia na kukupa makadirio ya gharama.