Huduma /

Upimaji wa Wingi wa Maji (Pump Test)

Tunapima kisima kinatoa maji kiasi gani kwa saa, ili kuchagua pampu sahihi bila kukausha kisima.

Pump test inaonyesha uwezo halisi wa kisima: lita ngapi kwa saa, na jinsi kina cha maji kinavyoshuka na kurudi. Bila kipimo hiki, ni rahisi kufunga pampu kubwa kupita kiasi inayokausha kisima, au ndogo isiyotosheleza mahitaji yako.

Hatua za kazi

  1. Kufunga pampu ya majaribio
  2. Kusukuma maji kwa muda maalum na kupima kiasi
  3. Kupima kushuka na kurudi kwa kina cha maji
  4. Ripoti na pendekezo la pampu

Omba Huduma

Tuko tayari

Unahitaji kisima cha maji?

Tuambie ulipo na unachohitaji. Tutakupigia na kukupa makadirio ya gharama.