Milan Hydrotech ni kampuni ya Kitanzania yenye makao makuu Mafinga, mkoani Iringa. Tunachimba visima vya maji kwa mashine kubwa za kisasa na kutoa huduma zote zinazohusiana na maji ya ardhini.
Kazi yetu huanza na utafiti wa maji ardhini unaofanywa na mtaalamu wetu wa jiolojia ya maji (hydrogeologist), ili kuchimba mahali penye maji ya kutosha. Baada ya uchimbaji, tunapima wingi na ubora wa maji, tunafunga pampu za umeme au za solar, tunajenga minara ya tenki, na tunakarabati visima vilivyoharibika.
Tunahudumia nyumba binafsi, mashamba, shule, taasisi, makanisa na misikiti, viwanda na jamii katika mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa, Dodoma na Singida.
- Tangu: 2024
- Mkurugenzi: Godfrey S. Mwambage
- Ofisi kuu: Mafinga, Iringa, Tanzania
- S.L.P: 655, Iringa

Timu Yetu
Watu wanaofanya kazi yako.
Godfrey S. Mwambage
Mkurugenzi Mtendaji (CEO)
Beatrice Godfrey
Imani Mwamlenga
Mtaalamu wa Jiolojia ya Maji
Abdalah Msimbe
Fundi (Technician)
Denis Urasa
Fundi (Technician)
Mikoa Tunayohudumia
- Iringa
- Njombe
- Mbeya
- Dodoma
- Singida
Uko nje ya mikoa hii? Tupigie, tutaangalia namna ya kukufikia.
Tuko tayari
Unahitaji kisima cha maji?
Tuambie ulipo na unachohitaji. Tutakupigia na kukupa makadirio ya gharama.


